Piczo

Log in!
Stay Signed In
Do you want to access your site more quickly on this computer? Check this box, and your username and password will be remembered for two weeks. Click logout to turn this off.

Stay Safe
Do not check this box if you are using a public computer. You don't want anyone seeing your personal info or messing with your site.
Ok, I got it
see ya!!!
Amekuwa binti wa miaka saba sasa na Janet anaonyesha uwezo mkubwa sana darasani kimasomo.Pia haachi kuwashangaza walimu na wanafunzi wenzake kwa kumudu kuongea lugha mbali mbali bila kujifunza.

Baba na Mama wa Janet wanapata mshituko pale binti yao anapokuwa mdhaifu sana.............Mama leo nahisi kuumwa ila najua ni ujumbe kutoka nyumbani.yalikuwa ni maneno ya Janet akisema atapata ujumbe toka kwao ambapo wazazi wake hawakuelewa kauli hiyo.

Sheshe ni kijana wa miaka 9 na wazazi wake walimchelewesha shule,ni kijana ambae kiumri ni mkubwa kuliko wanafunzi wote wa darasa la kwanza pale shuleni asomapo Janet.
Amejaliwa kipaji cha kuwa na akili nyingi na kuelewa haraka anapofundishwa.kila siku Sheshe alikuwa anamchukia sana Janet kwani kila alipofanya jaribio au mtihani basi alipitwa na Janet ana alishika nafasi ya pili.

Baba shuleni kuna msichana ananisumbua sana.Kila nifanyalo siwezi kumpita kimasomo na hata tukiwa tunajadiliana pamoja nae hunicheka na kusema mimi mjinga.........alikuwa ni mtoto Sheshe akimtuhumu Janet kwa baba yake.

Miaka 23 sasa imepita na Janet kawa binti wa haja.Anapata kitu katika maisha yake ambacho hata akimwambia mtu itakua anacheza tu kwani ameaambiwa iwe siri yake na akimwambia mtu matokeo yake atayaona.

Nakupenda sana Janet .......Sheshe alimwambia Janet.Moyo wa Janet haukuwa na hisia zozote za kimapenzi juu ya Sheshe kwani alijua wazi ni vijana wengi wanampenda ila hakuwa na ujanja wa kukubali au kukataa kuwa nao kimapenzi.

Akiwa ndani ya daladala Janet alipiga yowe na kupoteza fahamu.Akiwa hana fahamu aliona mambo ya ajabu ajabu akiwa sehemu yenye baridi sana na watu wa sehemu hiyo wapo uchi kana kwamba hawasikii baridi ile.wana manyoya mwili mzima na wana jicho mojamoja kila mtu,sikio moja na pua yenye tundu moja.Waliongea lugha ambayo Janet aliielewa vizuri sana lakini ahikikuwa kiswahili.Walikuwa wanatisha watu wale ila cha kushangaza Janet hakuwa na hofu yoyote.

Maria,mama yake Janet katika maisha yake alipenda sana ushirikina.kila alipopata tatizo dogo tu alikimbilia kwa wachawi wa jadi....mh ngoja niwaite madaktari wa jadi maana najua hawa huwa hawapimwi.

Katika kuhangaika na maisha,siku moja mama yake Janet alikwenda kutafuta dawa ya kupata mtoto kwani alishakuwa katika ndoa yake na mumewe kwa miaka 4 bila hata kupata mimba.

Keti hapo mama na nitakuangalia na kukwambia matatizo yako kama ni ya kweli sema "tawile dokta"kama si ya kweli usisite kusema.Haya toka tena nje kisha urudi ndani......................alisema dokta huyu wa jadi akimpa maelekezo mama yake Janet.

Katika hali ya mshangao alikuja Jirani yao Janet kule sehemu alipo.Huwezi amini alivyoonyesha ukarimu na kumkaribisha Janet katika makazi yake ya milele.alisema mzee Shabani........karibu sana binti,karibu Janet na hapa ni kwako.Mimi nimeshazeeka na hawa wote walikuchagua wewe.
ila masharti ya kazi yako ya uongozi wa nchi hii ni magumu sana.

Unataka mtoto wewe mama......tawile akajibu Maria mama yake Janet,na mumeo ni dume hasa ila mnamatatizo kwenye ukoo wenu wewe.........tawile baba...akasema Maria,na matatizo haya yatakuwa makubwa sana kama utapuuzia haya nitakayo kwambia.

Akachukua kibuyu chake Fundi huyu wa kweli sijui au wauongo mimi sina imani na hawa watu.akapuliza kikatoka moshi mwingi sana.kisha akachukua karatasi na kuweka vitu fulani akamwambia mama Janet....."sasa angalia kwamakini kama kutatokea sign yoyote basi ujue utahitaji matibabu kwangu tu na ni magumu pia kuyatimiza

Mimi aliuliza Janet ..........akajibiwa ndio mkuu na huna ujanja kwani inakupasa kikombe hiki alichokupa mama yako ukinywe.Na kuanzia leo hutakiwi kufanya mapenzi na mtu yoyote yule,isipokuwa watu sisi wajakazi wako na ukikiuka amri hii utapata mateso sana katika maisha yako na hutakufa milele.

Pili inakupasa kuwa makini kwani ukimnyooshea mtu kidole atapata maumivu makali sana na anaweza kufa,kwahiyo mnyooshee kidole mtu ukiwa unataka kumuua au kumtesa kwa namna fulani.

utaishi na watu duniani kama kawaida ila hawatakujua kama wewe ni boss wetu na hawatajua wewe ni nani labda uwaambie mwenyewe na ukisema basi utapata maumivu makali kwa muda wa miaka 700.

Mganga yule alieitwa Jigajigamajinijia aliweka pottasium pamanganet kwenye karakasi kisha akachanganya ny grycellin jelly.Kwa wale wasomi au wanasayansi wanajua reaction itakayotokea hapa.Basi kamlipuko ka kushtua kakatokea na ndipo Jigajigamajinijia akasema sasa kwanza inabidi ufanye mapenzi na mizimu yangu kisha ukafanye na mumeo siku hiyohiyo.

Mama Janet akakubali kwani alikuwa na shida ya mtoto...........masikini mizimu ya mganga yule kumbe ni mganga mwenyewe.Akammega kisawasawa mama Janet,akamfanya vitu hata mumewe hakuwahi kumfanya masikini.kisha Maria akatoka na kwenda kwake akamalizia na mumewe kama alivyoambiwa.

Haikuwa ni mara ya mwisho kwa mama Janet kwani alihangaika sana kwa wachawi.kila alipoona tangazo basi yeye akajua pale ndo atapata msaada.alipoteza pea nyingi na kuambulia kufanya mapenzi na wanaume wengi wasiona idadi.Wakati anafanya hayo mumewe hakuwa na taarifa na hakujua lolote kwani alikuwa ameridhika na hali ile.

Alipopata fahamu Janet alijikuta yupo hospitali na akiwa amezungukwa na ndugu na jamaa zake..........hakuna shida nahisi ni hali ya hewa tu .........alisema Janet.

Ghafla akaanza kukumbuka yale aliyoambiwa kana kwamba ilikuwa anaota na sasa akaona maandishi ukutani,yakirudia maelekezo yote aliyopewa kule na watu wake wale.Mama yangu sasa nimekwisha,sijui nifanye nini mimi jamani na sijui nitakuwa mgeni wa nani dunia hii.........Janet alijikuta akisema kwa sauti mbele ya watu waliomzunguka.

Mama mimi nina dawa ambayonikikupa utapata mtoto na atakuwa mwerevu sana..........alisema mzee mmoja wa kifipa...kutoka sumbawanga alieitwa Pikasebo.
dawa hii mama ni nzuri sana ila masharti yake magumu sana mama.nikikupa hapa usiangalie mtoto yoyote hadi unafika kwako,ukifika usionane na mumeo hadi ameenda chooni,akitaka mapenzi mpe ila anatakiwa afanye na wewe akiwa usingizini.
Utaweza mama?...........aliulizwa Mama Janet..........nitajaribu!jibu hili lilimshtitua sana Pikasebo na akaona ni heri amuulize tena mara ya 2.

Ndio maisha ya Janet yalivyokuwa,hana raha na anafanya kazi Bank lakini pesa zote anatoa kwa watoto yatima kwani haruhusiwi kutumia pesa hizo.anatamani kuwa na gari lakini haruhusiwi kabisa kuwanalo na vitu vingi sana alikatazwa Janet kutumia.

Mtoto huyooooooooooooooooooooooanakuja namhisi kabisa,ila fuata masharti mama ni muhimu madhara ya uvunjaji masharti ni magumu alionya sana tena sana Pikasebo mganga mashuhuri sana wa wanawake wasiona watoto au wesio na uwezo wa kuleta watu duniani.

Alipokuwa anaondoka Maria alisikia kishindo na kugeuka alikuwa ni Pikasebo.......mganga wake ameanguka.akajaribu kumuinua akashindwa.wakaja watu wakamchukua na kumpa huduma ya kwanza lakini ikawa wamechelewa kwani Pikasebo alishawatoka.Si ndio akatokea mama mmoja na mtoto analia sana?Si akageuka kumwangalia?!!!!!!!ikawa ameshavunja sharti la kwaanza na akawa anajuta sana.

Kwikwi na majonzi siku ya tatu,chakula hakipiti kwa koo kwani anajua sasa ni muda wa kusubiri maajabu tu kwani alijua wa kumtibu hayupo roho yake ishakwenda kwa ahera.
Baada ya muda akahisi ujauzito na ndio akazaliwa Janet........dadaa Janet mwenye kutuletea visa hivi hapa mtaani kwetu.

Hiyo ndio sababu ya kuzaliwa Janet na mzee yule aliehisi ni Jirania ambaye walikutana kule mlimani sehemu ya ajabu ndie Pikasebo mganga aliye mtibu mama yake na kufariki.

Hakuwa tu na roho ya kiajabu ajabu bali alikuwa pia na roho nzuri sana ya kibinadamu.akiwa amejipumzisha ...Janet anapata usingizi na kuota ndoto juu ya kijana mmoja atakae kutana nae jioni ya leo.Ni kijana anaevutia sana na hamfahamu.

kama alivyoota Janet akiwa kwenye daladala anashangaa kuona mtu anamkanyaga mguu wake tena kwa nguvu mno,oh samahani dada pole sana.alisema kijana mmoja mtanashati na buheri wa afya........nikimaanisha hana ngoma..je wewe umepima?
Ajabu ni kwamba kwa kukanyagwa kule Janet alitoka damu nyingi na ilimlazimu kijana yule kuchukua tax kumuwahisha Janet hospitali.

Naona maendeleo sio mabaya kwani maumivu yamepungua sana na pana pona sasa.alikuwa ni Janet akitoa maelezo kwa yule kijana alikuja kumsalimia nyumbani kwao.na ndie yule aliemkanyaga.
Naona leo ni siku ya 3 na hatujuani hata majina dada kuna ubaya kufahamiana maana naona urembo wako si haba na mimi nataka kufahamu undani wako bibie........alihoji kijana yule.

si vibaya go ahead!alijibu Janet huku akiwa na hofu na mota wa mapenzi ukiwa umeshawaka katika moyo wake...............-Naitwa Samson na ni mtoto wa kwana na wakiume pekee katika familia ya mzee Duima.Nafanya kazi TRA na sijaoa wala sina mchumba.
.........kazi kwako sasa huku akitabasamu Samson aliependa kuitwa SAM.Naitwa Janet......ni mtoto pekee wa Maria mama yangu mpendwa.nafanya kazi Bank lakini hainifurahishi sana,natamani kuwa na marafiki wengi,sina mume wala mchumba......alimaliza Janet huku moyo wake ukiwa kama unahisi kusaliti kitu fulani hivi?
Wazee kule dunia mafichoni waliamua kumchukua mtoto wao kumpa kozi mpya ili afuzu vizuri hasa ukizingatia sasa Janet ni binti mkubwa,walimchukua kimazingara na kumleta eneo la tukio.

Wewe sasa umetumikia vema upeo huu wa watu muhimu na hatari sana.Unajua bila mimi wewe usingezaliwa na Mama yako nilimsaidia nikijua naleta mtu muhimu katika dunia ya watu wema.Alisema mzee Pikasebo ambaye ndie alimfanya Maria mama wa Janet kupata mimba.

Samson baada ya mizunguko yake ya siku,na baada ya kukosa simu ya Janet kwa muda wa masaa takribani 4,aliamua kwenda kwa Janet ili kumjulia hali.Alipofika alikuta Janet amelala fofofo kana kwamba alikuwa na hangover ya mizinga 6 ya chimpumu.

Janet alirudi dunia hii tuishiyo mimi na wewe akiwa na roho tofauti kabisa kwani sasa amepewa umalkia na anaweza kufanya lolote na wazee wake kule dunia ya chini wasifanye lolote.

Kijana mmoja jina lake Tino,huyu alipenda sana kujirusha muziki,pombe hakugusa kabisa kwani hakuona umuhimu wake.Yeye alikuwa ni sigara sana na wanawake tu.Siku moja aliamua kwenda disko ikiwa kama saa 7 usiku baada ya kukosa usingizi kutokana na kelele za ugomvi wa jirani yake.

Akiwa njiani peke yake aliona kundi la madada poa pale maeneo ya kinondoni makaburini lakini yeye kwa kuwa hakujali basi alitembea taratibu kuelekea kituo cha daladala.

Janet malkia wa mizuka ya bahari na nchi kavu aliamua kumpenda sana Samson.Aliahidi moyo wake kutomfanyia mambo ya ajabu na wakawa pamoja kila ilipobidi.Janet alivunja mwiko kwani alihisi kumpenda kaka mmoja ambaye ni dokta pale muhimbili hospitali.Akaenda hku akijidai ni mgonjwa wa tumbo.

Dokta mimi tumbo linauma sana hapa...hapa dokta..akamuonyesha chini kidogo ya kitovu huku kitovu chake kilichotobolewa na kuweka kipini cha silver kikionekana.

Tino alitembea taratibu kuelekea kituo cha basi lakini hakufika...alishangaa ni nini kinaendelea alkini hakujua.Kila alipoangalia mbele aliona kituo kipo kama mita 8 to kifika lakini kwake kufika kituoni ilikuwa ni ndoto.Akageuka ili arudi nyumbani kwani alihisi kuna kamchezo kanaendelea au bado yupo ndotoni lakini alipogeuka nyuma anakumbana uso kwa uso na mrembo mmoja alieumbika kama malaika.

Moja ya kazi alizoamua kufanya Janet sasa ni kutimiza matakwa ya wazee kwani kuua kwao ilikuwa ni jambo la kawaida na kwasababu Janet alikaa miaka mingi bila kuwa na mpenzi basi aliamua kufungulia bomba kwani sasa alikuwa na mamlaka ya kuweza kuwamudu wale wazee wote wenye kiburi kule dunia ya chini.

Umeoa wewe dokta..aliuliza Janet aliebadilika na kuwa si mgonjwa tena.....sijaoa mama kwani vipi ...aliuliza yule dokta.
Jina lako nani wewe dokta...alihoji Janet..Naitwa Hamza.Ok unaweza kuja eo jioni pale msasani club nina maongezi na wewe kaka Hamza.

Tino hujambo,alimsabahi yule mrembo huku Tino riho ikimdunda kama inataka kutoka.Tino alibaki ameduaa huku jasho likimtoka kama maji..si..si..sjambo alijibu Tino kwa kigugumizi kwani alihisi kupenda ila alihisi mashaka makubwa sana moyoni.Unaelekea wapi saa hizi kaka?Aliuliza mrembo yule kwa shuku kisha akamwambia naweza kwenda na wewe kaka?

Kwakweli dada mimi nina shift ya jioni leo na kesho,halafu kuanzia kesho kutwa nitakuwa na wazazi nyumbani nikifanya mipango ya harusi yangu.Masikini dokta hakujua kama maneno hayo ni mwanzo wa chuki kati yake na Janet..Janet alibetua mdomo wake na kuamka na kuondoka.Hakufungua mlango ila alitoweka huku mlango umefungwa.

Tino akiwa anajiuliza yaliyo mpata aliona Tax inakuja akasimamisha na kuomba apelekwe nyumbani kwani alihisi yule dada ni changudoa hivyo akapanda tax na kuelekea kwake.Akiwa njiani ghafla anamuona yule dada aliekutana nae amekaa pembeni yake na anamwambia ama zake ama zangu.

Hakuna aliejua haya ayafanyayo Janet.Siku moja roho ikiwa imemtulia sana Janet alimuomba Samson amsindikize kwa mama yake.Walipofika walikaribishwa na kuketi kama ada.Kabla ya kuondoka Janet alimtambulisha Samsoni kwa mama yake kisha akaomba faragha na mama yake..mama usimwambie mimi nilipatikanaje halafu unajua kumbe mimi ni mzuka wa mtoto wa yule mganga aliekufanya unizae kwahiyo hii ni siri kubwa kwani ukumwambia nitaishi kwa aibu kubwa.


Nasikia ukitembea na mfupa wa nguruwe hupati visanga hivi.Lakini mimi nasema wewe mwamini Mungu tu na utaona maajabu makubwa.

Masikini dokta alikuwa anasubiriwa na watu lundo hapo mlangoni kila mmoja akilalamika bila kujua nini kinaendelea huko ndani.Jamani mapenzi si ofisini jamani huyoo mrembo atakuwa si mgonjwa labda kimada wake....alisikika mama mmoja mwenye lafudhi ya kitanga akibwabwaja kwa hasira.

Baada ya muda alikuja dokta mkuu pale kazini na kuingia chumba cha dk Hamza na kumkuta kaiwa amepoteza fahamu na yupo peke yake.wakamchukua hadi chumba cha wagonjwa mahututi akiwa hajitambui kabisa.Mchome sindano ya kutoa sumu labda kuna mtu amempa sumu...alisikika nesi mmoja akitoa ushauri alkini kama miujiza alitokea dada mmoja akiwa na baibui na kusema..mkimchoma sindano mmemkosa kisha akatoweka.

Janet alianza visanga vingi na kwa uwezo alionao aliweza kugona wachawi hata mchana.

Ghafla Janet alimwambia Tino na mimi nitakuonyesha leo mambo ya ajabu sababu unajifanya kiburi ona hii...Janet alimuonyesha Tino miguu..aah Tino akazimia ...aliona miguu ya Janet ikiwa na kwato kama za punda na alipopata fahamu alikuwa hospitali.

Maisha ya Janet ndo hayo ya kubadilika sura na kufanya mauzauza kila kukicha.Siku moja laisahau kama yupo na Samsoni akaanza kufanya mambo yake.Tulale bwana mpenzi ....alisema Janet.Ok ngoja nikazime taa...alijibu Samson lakini kabla hajaamka Janet alinyoosha mkono toka kitandani na kuzima taa.

Madaktari walishtushwa zaidi baada ya kumuona dokta Hamza kama ambaye amezini na mwanamke kwani alukuwa na kondomu kwenye uume.Lakini kabla hawaja taka kumtibu hakuwa nayo hii imetokea ghafla tu.

Taratibu Samson akaanza kuwa na hofu juu ya Janet na baadhi ya watu wakaanza kuzungumzia juu ya binti ambaye anamiujiza tele duniani.

Kuna mhubiri mmoja laikuja toka Denmark akawa anatoa neno la bwana kwa watu wa eneo lile.Akasema wenye shida mbalimbali wakaombewe,watu wengi sana walienda na Janet akiwa mmoja wapo,laikini yeye hakuwa na nia ya maombizi bali alienda kushuhudia ni nani huyo atendae maajabu zaidi yake.

Kuna mgeni hapa nimevuviwa na roho wa bwana,mgeni huyu ni wetu na tumpokee,anamatatizo ya kimapepo na anahitaji msaada mkubwa.Mhubiri huyu alisema hayo akiwa na uvuvio toka juu kwamba pale kuna mtu hatari sana na inabidi aombewe na uwepo wa Mungu inabidi uwepo yani watu wawe na imani.

Dokta Hamza alipata fahamu na kujikuta yupo juu ya mti mkubwa wa mbuyu,pembeni yake yupo Janet akiwa na sura ileile lakini chini anakwato na kucha zake zikiwa kama za mwewe.
Nakuambia nakupenda wewe unaringa..sasa ona upo wapi wewe...na sasa kuanzia leo ni marufuku kuwa na mwanamke zaidi yangu..utafanya mapenzi nitakapo mimi kama unabisha basi jaribu.Kisha Janet akamrudisha Hamza duniani.

Pale hospitali hapakukalika kwani Hamza alishtuka kama amepigwa shoti ya radi..halafu akakojoa mkojo mwekundu kama damu.Akaanza kuwaelezea watu juu ya yaliyomkuta kule dunia ya maajabu..akiwa anahadithia Janet akamtokea ila akawa anamuona peke yake tu...wengine hawakusikia hata sauti.........huyuuuuuuuu...huyuuuuuuuu amekuja tena jamani...kimya alimwambia Janet.nimekwambia usimwambie mtu na wewe hujasikia sasa endelea.

Samson anahofu sana juu ya alichokiona kwa Janet anaogopa kuuliza....lakini anasema kwa utani huku giza likiwa limetanda sana chumbani....umesomea mazingaombwe nini honey?masikini angejua ylivyo Janet asingethubutu kulala nae hasa gizani kama vile...

Ghafla mchungaji yule akapaliwa na akaomba maji anywe.Akakohoa sana ...akasema ni majaribu haya na Mungu atakucho...kabla hajamaliza akakohoa tena lakini nadhani alitaka kusema Mungu atakuchoma moto.
Wasaidizi wake wakiwa hawajui la kufanya wakashangaa kuona biblia ikiwa na damu huku mikono yao ikiwaka moto.wakiweka biblia zao chini moto unazima mikononi mwao wakibeba tu unawaka tena.

Mimi pia nilikuwepo pale na kwasababu sikujua mambo ya Janet basi nilihisi ni uwepo wa Mungu basi nikasema sala hii....
NAKUSHUKURU BABA..BWANA WA MBINGU NA NCHI..KWAKUWA MAMBO HAYA ULIWAFICHA WENYE HEKIMA NA AKILI UKAWAFUNULIA WATOTO WACHANGA.na wewe sema sala hiyo ili Janet asije akaja kwako,anaweza asije kama Janet walakini akaja kwa njia tofauti.


    Maisha ya Janet yalijaa mikasa na vimbwanga kibao.Ilifika wakati ambapo Samson yalimshinda mauzauza ya Janet na Janet alishindwa kujizuia kutofanya mauza uza wakiwa pamoja na Samson.

          Samson,aliita Janet..unajua mimi nina siri moja katika maisha yangu ambayo nadhani ni bora nikwambie tu...
Wakati mama yangu ameolewa...hakuwa na uwezo wa kupata mtoto.Alianza kutoa story hii ambya kwa Samson ilimfanya kama mwehu kwani alijua sasa ndio anaona maajabu.

          Mama yangu aliogopa kuachwa na baba yangu hivyo alienda kwa mzee mmoja...wakati Janet anaongea maneno yale,Samsona ukampata kama usingizi hivi kisha akaanza kuona mambo ya ajabu ajabu sana.Aliona watu wengi waliokufa zamani na alimuona Janet akiwa katika mavazi yanayo waka kama mshumaa.

          Karibu Malkia wetu,alisikika mzee mmoja akimkaribisha Janet kwa heshima sana.Huyu ni Samson na ni mchumba wangu.alisema Janet kwa kujiamini sana.Nimeona nimlete huku aone mambo nifanyayo na asishtuke siku nyingine atakapoona mamboyasiyo ya kawaida kwake.

        Yule mchungaji aliendelea kuteseka kwa kushindwa kupumua na aliona kama sura ya mwanamke ikiwa mbele yake na alishindwa kumtambua kabisa.....msichana yule alikuwa ni Janet ambaye alitaka kumuonyehs akwamba yeye ana nguvu kuliko imani ya mchungaji yule.

        Wana maombi maalum walikaa kumuombea mchungaji na ghafla Janet aliamua kuondoka eneo lile akimuacha mchungaji akiwa hoi kwa kichapo alichompa.Yeye aliona amefanya jambo lenye maana sana na alijipongeza kwa hilo.

        Akiwa anaendelea kushangaashangaa kule ndani alitokea mzee mmoja ambaye ndie alikuwa mganga wa mama Janet na ndie aliye mletea Maria mtoto aitwae Janet.Hujambo kijana? aliuliza yule mzee huku akimwangalia sana Samson.Huyu anatufaa sana maana ana roho ngumu sana huyu.Halafu ana imani kali sana juu ya huyo wanaemuita Mungu lakini atakuwa mtu muhimu sana kwetu..alisema mzee yule huku akimpigapiga Saamson begani.

            Samson alishtuka sana kusikia maneno yale lakini hadi wakati ule hakua na uwezo wa kuonge lolote.Alikuwa kama anayeota ndoto ndefu halafu anaikumbuka sana.Aliona maajabu ambayo hakuwahi hata kusikia katika maisha yake na alianza kujuta kumpenda Janet.

        Daktari mmoja anaitwa Hizza alihoji kama kuna uwezekano wa kumchukua Dokta Hamza ili akamfanyie uchunguzi...Alipenda sana mambo ya kishirikina huyu na alikuwa na imani kabisa kwamba Mwenziwe huyu amerogwa na ama daktari mwenzake au mchawi jirani yake.

        Aliamka Samson akiwa kama kapigwa shock ya umeme kwani aliruka juu na kuanguka chini kma gunia.Nadhani hutakuwa na swali maana nilijua nikikupa story bila kuona ungekuwa na mswali mengi sana....alisema Janet huku akiwa amemkazia macho sana Samson.

        Ama kweli dunia hadaa na walimwengu shujaa...alisema Samsoni akiwa hana la kuongeza masiki mtoto watu.Kwahiyo hata siku ile ulipozima taa ukiwa kitandani ulikuwa unanionyesha vituko?aliuliza Samson kwa woga mkubwa sana huku akiwa amelowa jasho.

          Samson alipanga njia ya kumtoroka Janet na siku iliyofuata alienda kituo cha basi na kwenda kwao kijijini.Alimuhadithia babu yake mkasa wote na babu bila ya kusubiri alimpeleka Samson kwa mzee Kidawa ambaye aliaminika sana pale kijijini kwa kutoa tiba za jadi.

        Alipowaona tu mzee kidawa alianza kuumwa na kichwa.Jamani ugeni huu siuhitaji mimi..siyawezi mambo yenu tafadhali kijana.Nomba sana mniache maana nimeona dalili mbaya jamani ondokeni.alisema mzee kidawa huku akishika kichwa na kuguna kwa maumivu makali sana.

        Usiku kabla hajapata usingizi vizuri,Samson alimuona Janet akija na kumshika mkono.Ulijidai mjanja eeh,hapa basi umefika na mimi ni mjanja zaidi.Nilikwambia usithubutu kunikimbia wala kutembea na mwanamke sasa wewe unadhani natania eheee.Haya funga kila kilicho chako tuondoke.Samson alipiga kelele sana na watu wakaja chumbani kwake na kukuta hayupo.

        Janet alimpeleka Samson juu ya mti mkubwa na kuamua kumuacha hapo.ulikuwa usiku mzito na Samsona aliogopa sana na asijue la kufanya.Alitafuta njia ya kurudi nyumbani asiione kabisa.Akaanza kulia kama mtoto.Alipogeuka nyuma aliona watu takribani kumi hivi wakiwa wamevaa mavazi meupe na meusi na walikuja harakaharaka kama wanamfukuza mtu.

          Wana maombi wa kanisa la yule mchungaji toka Denmark waliendelea na maombi huku yule mchungaji akiwa na afya nzuri kabisa.wakafanya sala ya pamoja na kuamua kuiombea nchi nzima dhidi ya ushirikina na mapepo mabaya.

        Kama unadhani unaweza kufanya lolote basi fanya hapa,maana watu watadhani wewe ni mshirikina kama utaanzisha mada za ajabu ajabu...alishauriwa Hizza na daktari mwingine na yeye akachukua ushauri huo kama alivyopewa kwani ulikuwa wa busara na ulikuwa na lengo la kuepusha imani za ajabu pale kazini.

          Jamani mwenzenu nimeona maajabu sana..alisema dokta Hamza baada ya kupata nafuu.Alikuja binti mmoja kama mgonjwa na aliingia ofisini na nikaanza kumsikiliza kama ilivyo ada.Cha ajabu alisema ananipenda na alitaka kukutana na mimi jioni ya siku ile.

        Akiwa anaendelea kuhadithia alikuja nesi mmoja akiwa amejifunga ushungi,hakuna aliyeshtuka kujua ni nani bali alisalimu kisha akasema..huyu kijana haumwi jamani mwamsheni.Kila mtu aligeuka kumwangalia na hakuwa mtu waliemfahamu.Na walipata mshtuko baada ya kumuona na ushungi kazini.

          Walipoangaliana na kumgeukia tena yule nesi alitoweka machoni mwao na kuwaacha wakishangaa na kulizana maswali mengi.Jamani naona hapa kazini tumeingiliwa sasa jamani..alisema kijana mmoja ambaye ni mfipa...we si mfika bwana?yawezekana umeleta haya mambo alisema mzee Shaka ambaye ni mtu mzima sana na amebakiza miezi tu kustaafu.

      Nimefanya kazi miaka 59 na miezi kadhaa sijawahi kuona mauza kama haya jamani.Ila nawashauri kumuomba Mungu kwa bidii,Kizazi hiki kina mitihani migumu sana ya Maisha.Nadhani ni kutokana na imani zenu na mmomonyoko wa maadili...alisema mzee huyu na kuondoka zake.

          Samsona aliendelea kuona watu wale wakija na walifika hadi karibu na yeye kabisa.Kijana unatukumbuka lakini?Leo tumekufuata hadi hapa na tunadhani hapa ni mahali panapo kufaa zaidi.Tunakuonya tu kwamba ukijaribu kwenda kwa waganga watakufa mmoja mmoja na wewe utakuwa asusa yetu.Baada ya kutoa vitisho hivi waliondoka na kumuacha Samson akiwa bado analia na kusaga meno.

          Huruma fulani hivi ilimuingia Janet na akaona ngoja akamfuate Samson na kumrudisha nyumbani....Umekoma sasa eeh..umeamini mimi si wa mchezo sasa eeh?Haya fumba macho sasa na alipo ambiwa afumbue alijikuta kwao.

          Alishangaa kuona mambo tofauti kama yalivyokuwa zamani kwani watu wengi ni kama hawakumuona njiani.kila aliposalia watu wengi hawakuitikia na alianza kuona watu wengine wakiwa uchi na wengine wamebeba viungo vya watoto wachanga.

        Siku hizi utakuwa unaona mambo mengi sana ya dunia hii.Usishtuke maana utaona wachawi na una uwezo wa kumshuru mtu yoyote kwa kumnyooshea kidole tu.Karibu sana kwenye himaya yangu Samson.alimaliza kusema Janet nikiwa sijui nijibu nini.

        Samson alitaka kujaribu kama kweli anaweza kumdhuru mtu na alimnyooshea kidole Janet,bila kujua kama yule ni malkia wa wale mashetani,Janet alipata msukosuko kidogo na kuanguka chini.Hahahaha kijana mdogo sana wewe..mimi ndio malkia wenu na naweza kuharibu na kurekebisha hali zote.alisema Janet kwa majigambo.

          Akiwa anawaza maisha yake ya shuleni Janet alimkumbuka mtu anaitwa Sheshe..huyu alimsumbua sana shuleni na aliwahi kumtaka kimapenzi...Sijui nitampata wapi huyu Sheshe?alijiuliza Janet huku akiwa amelala juu ya Samson mpenziwe.

        Kesho Samson nakupa asignment ndogo tu na ukishindwa basi ujue unakufa...alisema Janet huku akiwa amemkazia macho Samson.Nimekukosea nini Janet,ni mapenzi ya aina gani haya?nadhani yupo atakae kubali kuishi haya maisha ila mimi sitaki...Kama unaweza niue tu hata sasa hivi.Ni bora kufa kuliko kuishi maisha haya ya shida kubwa.alisema Samson akiwa amekata tamaa kabisa ya kuishi.

        Mauzauza ya Janet yalisha zoeleka mtaani kote na kila mtu   alimjua Janet kuwa ni mtu wa miujiza ya kishetani.Hii haikumpendeza sana Janet na alipanga kuhama mji.Na alipanga kuondoka na Samson.

      Bila kuaga ndugu zake Samson alijikuta mji wa ajabu sana.Wenyeji walikuwa wakarimu mno na hawakua wakivaa nguo..ikabidi Janet na Samsoni waanze maisha mapya kama wanyama wa porini.

      Mchungaji Benson alikuja Tanzania kutoka nchini marekani.Mchungaji huyu ana karama nyingi sana alizojaliwa na mwenyezi Mungu na alitenda mengi ikiwa ni pamoja na kuponya wagonjwa na kusaidia miradi mbalimbali na kutoa huduma nzuri kwa jamii

        Mchungaji huyu alikija Tanzania hasa baada ya kusikia kuna vijiji nchini humu ambapo watu hawamjui Mungu na havija staarabika bado na wanatumia bado mizizi   kwasana na hawana hata huduma za kijamii.Hivyo alijipanga kwenda katika vijiji hivyo ili kutoa msaada kwa kadiri ya mahitaji ya kijiji.
        Alianza kazi ya kutoa neno la Mungu toka kijiji kimoja hadi kingine huku akihamasisha maendeleo vijijini humo..alialika wawekezaji wengi nchini na kukaanza kutoa nuru kwa vijana wa vijijini na mijini.Vijana wengi walihamia vijijini hasa baada ya viwanda na mashule mengi kujengwa na wawekezaji wengi walioletwa na mchungaji Banson

      Alitembea vijiji vingi na aliona na kujifunza mengi pia.Akiwa kijiji kimoja alikuta watu wakiwa wanaishi kama wapo katika enzi za ujima kabisa..kwani hawakuwa wakivaa nguo na walikuwa hawajui shule ni nini na walipomuona Mchungaji Banson walianza kukimbia na kumcheka mtu huyu mweupe.

        Watoto walimuogopa na habari zilienea sana pale kijijini kuwa watu wa ajabu wamekuja.Kijijini hapo palikuwa na kijana mmoja tu aliesoma na alikuwa anaishi pale na mifugo mingi.Alisikia juu ya ujio wa wageni basi yeye akajua ni wageni wale wa kwanza yani Samson na Janet.

        Wakina Samson na Janet pia walisikia ujio wa mtu huyu wa ajabu akiwa na wafuasi wengi waliokuja nae hivyo walienda kumuona na kumsabahi.Sisi ni watu wa Mungu na tumekuja hapa kuleta maendeleo na neno la Mungu alisema Mchungaji Benson katika moja ya mkutano alioandaa pale kijijini.

        Hakuna aliye muelewa zaidi ya Janet na Benson..Wakati wote huu Janet alikuwa likizo ya vituko vyake na Samson aliwaza juu ya kuondokana na shida ya maisha yale aliyoiishi kama mtumwa.

        Siku moja akiwa amelala,mchungaji Benson alipata ndoto kwamba kijijini pale kuna watu wa ajabu sana na hawana huruma mbele ya viumbe wa Mungu.Alifunga kwa siku tatu bila kula na alianza kufanya hivyo ili Mungu ampe nguvu za kupapambana na miujiza hiyo ambya aliota ndotoni.

      Kweli Mungu wa ajabu kwani wakati wote huu Janet hakuwaza kumdhuru Mvchungaji Benson na alikuwa kama hajui kuna mtu mwenye upeo wa kusambaratisha nguvu zake za kichawi.

      Wakiwa wamelala   juu ya mti ambapo ndio yalikuwa makazi yao mapya yeye na Samson,.....Samson aliamka na kutoroka,safari hii alisema kama kufa basi bora afe kuliko kuishi maisha ya kinyama na kutenda uovu bila kudhamiria.Alifika sehemu moja na kukuta mahema na watu wakikesha kumuomba Mungu.

        Alisikia sauti ikimwita lakini hakujali..ikaita tena na tena lakini yeye aliendelea tu kufuata hema lile aliloliona kwa mbali.Kumbe aliyekuwa anamwita alikuwa ni Janet na aliogopa kufika eneo lile kwani alihisi nguvu zake za kichawi zinakwisha kadiri alivyozidi kusogelea eneo lile.

      Samson alifika kwa mchungaji Banson na akaombewa sana na nguvu zile za kishetani zikatoweka kabisa.Akajiunga na shughuli zile za kumtukuza Mungu huku akuwa na hofu kuwa ipo siku Janet atamfuata.

      Janet alipanga njia ya kumrudisha Samson bila mafanikio na laiti angekuwa na uwezo zaidi basi naona safari hii angemuua kabisa kwani aliamua kurudi mjini kumtafuta mtu aliehisi anampenda sana.

        Baada ya mchungaji Benson kusikia hadithi nzima ya Janet kutoka kwa Samson ...aliahidi kufanya maombi maalum ili Janet naye aokoke kama Samson.

      Janet alimpata Sheshe akiwa mjini anatafuta mahitaji yake na walipokutana walilakiana kwa shangwe...habari za siku nyingi Janet,mbona umepotea sana yani miaka zaidi ya ishirini ndio tunaonana leo?Nakumbuka nilikwambia nakupenda na bado nipo single na nitakupenda milele.alisema Sheshe akimwambia Janet na angejua nini kinafuata baada ya uhusiano wao asingetamani hata kukutana na Janet.

            Walianza uhusiano wao na wakatambulishana kwa wazazi na muda si mrefu wakafunga ndo wakawa mke na mume.Maisha yao yalikuwa ya furaha sana na Janet hakutaka kumhusisha Sheshe katika mambo yake ya utoaji roho viumbe wasio na hatia,bali alifanya mwenyewe na kwa muda wake.

          Wakiwa bado kwenye maombi makali,Mchungaji Benson aliamini kwamba roho mbaya itamtoka Janet na atakuwa mtu mzuri tu.waliendelea na maombia usiku na mchana na siku moja njiwa alikuja pale kwenye kanisa dogo lililojengwa kijijini pale na mch Benson.

        Njiwa yule alikuja na karatasi lililoandikwa maneno haya....BENSO SASA UPO HURU.SIKUHITAJI TENA KWANI SASA NINA MPENZI MPYA NA TUNAISHI KWA RAHA...LAKINI KUMBUKA IMANI YAKO IKICHUJA NITAKUFANYA KUWA SEHEMU YA KUWEKEA MIGUU NA OLE WAKO UMWAMBIE MTU JUU YA MAMBO YANGU.ilimaliza sehemu tu ya ujumbe toka kwa Janet ambao uliletwa na njiwa.

        Huwa naamini njiwa ni ndege wa amani na mjumbe mzuri..naomba mniletee huyo njiwa jamani..aliomba Mchungaji Benson.Kila walipojaribu kumkamata walishindwa na njiwa yule alisubiri majibu toka kwa Samson.

        Imani yenu bado haija komaa sawasawa jamani haya ngoja nione kama njiwa huyu ni wa amani au wa vita na nipo tayari kuikabili vita hii kwa Jina zito la Mwenyezi Mungu.Alipomkaribua njiwa yule alianza kutoa machozi na akaangua chini na kugeuka damu nzito sana.

        Baada ya muda damu ile ikaanza kujikusanya na kuwa kama kichuguu fulani cha damu..Ongezeni maombi naona dalili ya ushindi wa Mungu inaanza kuonekana sasa.....alisema mchungaji Benson huku akiwa na siku ya saba bila kula ...aliamua kufunga ili ashinde majaribu yale aliyoamini yanatoka kwa Janet.

        Baada ya siku kadhaa Janet alianza kuumwa sana na alikuwa anatibiwa bila mafanikio.Hakujua nini kinaendelea ila aliamua kufunga safari kurudi kule dunia ya ajabu ili kupata ushauri wa wazee.Alienda kimiujiza na kufika akakuta watu wa dunia ile wote wameangamia na ugonjwa kama wake.

        Ilikuwa ni usiku wa manane pale Sheshe alipoamka na kumkuta Janet ni wabaridi sana.Akamgeuza na kugundua Janet amefariki saa nyingi,akapiga kelele na watu wakaja na baada ya muda walizika.

          Siku kama saba baada ya mazishi ya Janet,Sheshe alienda kaburini ili kusali kwaajili ya marehemu mkewe.Alipofika alikuta watu wengine wakiwa wanazika karibu kabisa na kaburi la Janet.Alianguka na kuzimia baada ya kuona cheni na nguo alizozikiwa Janet zikiwa juu ya kaburi la Janet.Huo ukawa ni mwanzo tu wa maajabu aliyoyaona Sheshe baada ya msina wa Janet.

            Siku mija akiwa kazini alimuona Janet akija kwa mbali na nguo zilezile alizozikiwa,alitembea kwa madaha na kujiamini sana kisha akatoweka.Ghafla akatokea tena ofisini ila hakusema neno alikuwa analia tu.Kimya kimya Sheshe akazimia na karani wake alisikia kishindo kikubwa kuja akakuta boss wake amezirai.

            Mchungaji Benson alifanya mengi na yakushukuriwa sana pale kijijini na aliamua kumpa kazi ya uchungaji Samson ambye alifanya mengi na yakuaminika sasa.Aliamua kurudi mjini kwa mapumziko kidogo huku akimuacha Samson kama mchungaji wa kijijini ambacho sasa ungelinganisha na mji wa Mwanza kwa ukubwa na maendeleo yake.

        Kama haitoshi Janet aliendelea kumtokea sana Sheshe na aliamua kwenda kwa mama yake Janet kumpa taarifa hizi za kutisha.Mama Janet alimuonea huruma sana Sheshe na wakati wanaendelea kuongea habari za Janet ...aliibuka tena Janet safari hii wakiwa Sheshe na mama Janet.Ulisababisha wewe mama na msaidie sasa Shshe hana hatia huyu.alisema Janet na kutoweka.

        Sheshe alisikia juu ya mchungaji Banson na akaamua kumtafuta.Alimpata na akajiunga na maombi makali hadi akawaamua kuwa na yeye mchungaji.Toka siku alipojiunga na Mchungaji Benson,hakuwahi kumuona Janet tena hadi leo.
        Wote waliowahi kudhuriwa na Janet kwa njia moja au nyingine sasa ni wazima kabisa na wana afya njema.
kweli Mungu wa ajabu na huo ulikuwa mkasa wa Janet kama nilivyouleta kwenu kwa hisani kubwa ya Kitabu cha hadithi kiitwacho---------vipande vya moyo wangu uliovunjika------AMBACHO NIMEKITUNGA NA KIPO NJIANI KUKUJIA SIKU YOYOTE...KAMA UJIO WA JANET

------------------ADIOS-------------AMIGO--------------------
Take Me Home...