Stay Signed In
Do you want to access your site more quickly on this computer? Check this box, and your username and password will be remembered for two weeks. Click logout to turn this off.
Stay Safe
Do not check this box if you are using a public computer. You don't want anyone seeing your personal info or messing with your site.
Baada ya misukosuko yote hii,Magge naishi nae mke wangu tena mapenzi yamezidi sana kwake.....Baba nataka chips kuku..alikuwa ni mwanangu Jeremia aliyekuja mbio kuniambia anataka chips kuku.
Mama Jeremia,Leo twende tukale Hotel naona itamfurahisha sana Jerry.Ndivyo nilivyopenda kumuita mwanangu huyu kipenzi.
Kumbukumbu za maisha na mateso niliyopata kule swazi siwezi yasahau na ni kama hadithi ukimuhadithia mtu.Au kama sinema za Marehemu Van damme kabisa.Lakini sasa imebaki historia na maadamu mama watoto nipo nae tena nyumbani Tanzania,basi hakuna shida tena na nikutumia vizuri siku zetu za kuishi zilizobaki.
Atukuzwe Mungu milele............................Lbada nianze kukupa sasa nini kilinipata,mimi ni nani na ilikuwaje huko swazi
Naitwa John Makalo,ni mtoto wa kwanza katika familia ya mzee Makalo.Nilisoma shule ya majanini na kukulia hapo pia.Nimeajiriwa katika shirika la ugavi umeme nchini Swazi.
Maisha hapa yanaendelea vizuri sana na ninapata pesa za kujikimu na kusaidia ndugu zangu nyumbani Tanzania.Ninaishi peke yangu kwasasa japokuwa nina mpenzi ambaye ni mswazi na ananipenda mno nami nampenda kama lulu.Mungu akipenda tutafunga pingu za maisha mwakani kama tulivyopanga.
Mambo mengi hapa nchini ni mageni sana ukilinganisha na kule nyumbani Tanzania.Kwa kiasi fulani naikosa sana nchi yangu japo sina njia kwani hapa natafuta riziki tu na moyoni nimepanga kwamba baada ya kutosheka na kazi hii na baada ya kupata pesa za kutosha nitafunga virago kurudi nyumbani.
Nilikutana na Magreth ambaye mimi humwita Magge siku ya wageni nchini swazi.Hii ni siku ambayo wageni wote waliofika nchini pale mwanzoni mwa mwaka hukaribishwa na mfalme.Kama kawaida nilitinga kwenye tukio hilo nikiwa mgeni tu wakawaida na tulijitambulisha wageni wote kisha mfalmme aliongea sana juu ya nchi yake na mazingira ya kuishi hapa bila matatizo.
Baada ya Mfalme kuongea sana na kueleza ni kwanini nchi yake bado ina mfumo wa kifalme,tulipata nafasi ya kusakata musiki wa asili ya kiswazi na baadae tukapata vinywaji na chakula.
Nilishangazwa na ukarimu wa watu hawa kwani ni nadra sana kupata wenyeji wenye moyo mzuri kama hawa ndugu zetu.Nikiwa nasakata muziki,walikuja mabinti wawili mmoja anaitwa Magge na mwingine anaitwa Suzane.Suzzy alisema yeye ni mtanzania na ameolewa pale na alifurahi sana kuona mimi ni mtanzania.
Magge alijitambulisha kuwa yeye ni mswazi na anafanya kazi posta.Nilimuangalia mara mblimbili kisha nikasema jamani muziki huu mzuri tuchez kidogo.Nilizungumza kiswahili nikona Magge ameboreka sana kwani alitamani kuelewa sana nini nimesema ila hakujivunga kuuliza.
Ooh samahani sana Magge nilisema twende tukacheza mama..samahani sana..nilimwambia kwa lugha ya kiingereza na alinielewa sasa na akafurahi sana.
Unaambiwa jamani dada alikuwa ni mzuri sana..moyoni nikahisi hakosi mchumba huyu lakini nikasema pia mbona kaja peke yake sehemu kama hii?Dada Suzzy ..Magge ameolewa au ana mchumba?nilimuuliza Suzzy ambaye badala ya kunijibu alicheka sana na kusema...Magge hapendi tuongee kiswahili.Huyo hapo muulize ..alitumia lugha yakiingereza ambayo ilimfurahisha sana Magge na kujua nini tulikuwa tunaongea.
Nilishikwa na kigugumizi na kujikuta naongea kiswahili tena kwa Magge..hali hii hunipata pale ninapotaka kutupa nyavu kwa warembo wazuri na walioumbika kama Magge.
Yalikuwa ni maneno yaliyonipa furaha baada ya kusikia bibie Magge alikuwa hana mchumba na alikuwa akiishi peke yake katika chumba alichopanga pale mjini.Haki ya nani Mungu alitumia siku nyingi sana kumuumba huyu binti.Na alihakikisha hakosei hata kiungo kimoja maana ameumbika sana huyu mrembo.
Vipi kwani mbona umeniuliza hivyo jamani John?alihoji Magge,ah nilitaka kujua tu dada unajua maua mazuri uyaonapo shambni huna budi kuyafahamu kama huyajui..nilimjibu huku nikitabasamu.Hayo maua mazuri umeyaona wapi wewe John?mbona makubwa haya jamani...alisema Magge huku akimwangalia Suzzy
Dada Suzzy mimi mwenzio hapo ndo nimeshapenda ila najua ni mapema sana kutuma majeshi yangu kwa himaya hii inayoonekana kuwa ngumu kuivamia..nilimwambia Suzzy ili angalau aseme atanisaidia kuteka majeshi haya ya Magge.Suzzy alicheka tu na kukaa kimya.
Baada ya party ile niliondoka na kwenda nyumbani nikiwa nawazajuu ya Magge tu.nilitafuta mawasiliano nae bila mafanikio kwani muda mwingi simu yake ilikuwa inafungwa.Dada leo nataka niwaalike kwa dinner familia yako na Magge kama unaweza kumpata.Alikubali Suzzy kuja kwangu lakini Magge alikuwa busy sana siku hiyo hivyo alitoa udhuru na kusema angekuja siku nyingine.
Atafutaye hachoki na akichoka ujue kapata...niliendelea kumpigia simu magge bila mafanikio.Kila niki piga naambia mtumiaji wa simu uliempigia yupo sokoni kwa sasa au unaambiwa mtumiaji wa simu uliempigia anafua kwa sasa.Basi ikwa kama naongeza machungu moyoni maana nilihisi nimepewa namba ya uongo au ana mchumba na hataki kusema.
Nikiwa nimekaa bila kujua nifanye nini,siku ya ijumaa nilipata simu iliyoandika private.Mara nyingi simu hizi huwa sipokei lakini cha ajabu siku hiyo nilipokea...halooo,John hapa..nilisema.Hujambo John iliitikia sauti nzuri ya malaika wa kwanza kwanza huku duniani.Guess who is speaking ah bila kusita nikasema ni Magge wewe naye akacheka na kuuliza kama nitakuwa na muda kesho jumamosi.
Tulikutana Jumamosi na nikawanae kwa siku nzima,tuliongea mengi nikamuomba kama tunaweza kuwa wapenzi na akasema hilo nisahau kabisa kwaniana expirience mbaya sana na relations na ameshaamua kuishi peke yake.amechoshwa na wanaume maana ni wadanganyifu na si waaminifu kabisa.
Si wote Magge,halafu isitoshe hao walikuwa waswazi na mimi ni mtanzania Magge.Jaribu kuona kwamba kujumuisha wanaume wote katika kundi moja tena la waongo na wasio waaminifu unakosea sana tu na ni bora ukafuta dhana hiyo potofu ulioijenga kichwani mwako...nilimwambia.
Maneno yangu hayakumuingia kabisa akilini Magge na niligundua nilikuwa namkera na habari zangu.Unajua kwanini nazima simu muda mwingi?sababu ya wanaume..sijui wanapata wapi namba yangu na napata simu zaid ya mia mbili kwa siku na zote zikitaka uhusiano na mimi.Wapo waliowahi kunipa hadi dola laki moja ilimradi nilale nao tu na pamoja na umasikini wangu nilikataa kabisa.alisema Magge.
Hakika nimepatikana lakini sikati tamaa bwana mimi nitamsumbua sana hadi ataona umuhimu wangu kwake.Kwanini usinunue line nyingine tukawa tunawasiliana na mimi Magge?nilihoji na kuinuka na kwenda chumbani.Nakumbuaka nilikua na simu mpya ambayo ni nokia na sikupenda kuitumia kwani sipendi visimu vidogo.Na ilikuwa na line mpya pia nikamkabidhi Magge na kumwambia tumia simu hii kuwasiliana na mimi tafadhali ..sijawahi tumia namba wala simu yenyewe.
Alipokea na kusema asante kisha tukawa tunaongea mambo mengine tu huku nikitamani kurudisha story zile zinazonikera moyoni.Umeshawahi kupenda Magge?mapenzi yanauma sana kama unajua,halafu ukimpenda mtu na ukigundua hakupendi basi ndio inafanya mtu atamani kujiua kabisa...nilimwambi Magge.
Sio kama sikupendo John,nakupenda sana ila sipo tayari kuwa mpenzi wako jamani naomba unielewe.Naomba tuwe marafiki wazuri tu na tusaidiane kwa hali na mali kaka..au unasemaje...Aliuliza Magge huku hajui kama ananipa maumivu makubwa sana moyoni.
Ni kipindi cha miezi sita sasa imepita na tunawasiliana na kutembeleana na Magge kama kawaida.Kila nikimpigia simu nakumbushia mada ya kumpenda na anakaza uzi kama iziraeli vile.
Ndio maana nikasema ukipenda chongo utaita kengeza na kama una nia ya kutafuta kitu basi huchoki hadi upate.Ndivyo nilivyosema mara kwa mara kila nilipopanga nia ya kuuteka moyo wa Magge.Binti mkumu kama mti wa mpingo na anamsimamo kama rais wa cuba.
Siku moja nikiwa kazini nilipata matatizo kidogo,kibali cha kazi kilikwisha na nilisahau kukiongeza muda kwa muda wa kama wiki tau hivi.Baada ya ukaguzi niligundulika na polisi wakaniweka chini ya ulinzi.Alikuja Suzzy na Magge wakanitolea dhamani kisha nikaongeza muda wa kibali na kuwashukuru kwa wema wao.
Ilikuwa ni mwaka mpya ambapo nilimwalika Magge tusherekee pamoja.Alifika akiwa na kifurushi kikubwa kidogo.Alinikabidhi na kuingia jikoni.Umeandaa nini cha kupika kaka?Aliniuliza na kumwambia kuna chips na nyama nyingi tu kwenye friji.
Baada yakula tulianza kuweka pombe taratiibu sana hadi mida ya saa tau usiku.Nikaandaa mafataki yangu mawili kisha nikarudi pale varandani tulipokaa na Magge.Pombe zilianza kumkolea Magge na alikuwa stable bado.Akaanza kusemahili na lile huku zikiwa ni pumba tupu.
Saa tano na takika hamsini na tisa tukaanza kuhesabu sekunde hati kamili saa sita nikapiga mafataki yangu na kurudi ndani.Nimekuandali zawadi Magge ya mwaka mpya.Nikaenda ndani nikamletea box akaanza kulifungua.Alitoa kitabu cha hadithi za mapenzi ambacho hakujua kama mtunzi nilikuwa mimi kisha akachukua na coupon ambayo angeweza kufanya shopping ya nguo itakayo gharimu dola 500 za marekani.
Asante sasa kakana Mungu akuzidishie,akupe moyo wa uvumilivu bila kukata tamaa kama ulivyo.Unajua John wewe ni mtu wa ajabu sana.Yani hujakata tamaa hadi leo unaendelea kunifukuzia tu.Basi leo nakwambia rasmi.Pamoja na zawadi zako...guess nataka kukwambia nini kaka.alihoji Magge huku akicheka.Mimi nilijua sasa anavunja hadi urafiki kwani inawezekana hakupendezewa na zawadi zangu.
Pamoja na zawadi zako nzuri kaka...na moyo wanko wa uvumilivu,na ushujaa wa uaminifu..napenda nikwambie mimi nina mchumba tayari na ananipenda sana.Amekuwa mwaminifu na nilitumia muda mwingi sana kumchunguza kaka.Nilipigwa na butwaa na hili lilionekana waziwazi...hakuna shida Magge mpende sana..naona haukuwa mpango wa Mungu nilimjibu Magge huku nikiinamisha kichwa chini kama niliekosa pumzi ya kuishi.
Akaamka na kunikumbatia kisha akanibusu mdomoni na kusema...UNGEKEWA LULU NINGEZAMA MWAMBANI,
UNGEKUWA KIFARU NINGEHAMIA MWITUNI
UNGEKUWA SAMAKI NINGEKUVUA BAHARI
LAKINI UKO NAMI HAPA SIJUI NIKUFANYE NINI???alimaliza Magge kusema maneno yaliyopenya moyoni mwangu na kufanya furaha ya ajabu.
Basi tuka bebana ahdi chumbani tukapumzika hadi siku iliyofuata.Nilihoji kama Magge angependa kuhamia pale kwangu kwani nina nyumba kubwa halafu naishi peke yangu nae bila kusika alikubali kwa sharti kwamba ni lazima tufunge ndoa ndipo yeye anaweza kuhamia pale.