Stay Signed In
Do you want to access your site more quickly on this computer? Check this box, and your username and password will be remembered for two weeks. Click logout to turn this off.
Stay Safe
Do not check this box if you are using a public computer. You don't want anyone seeing your personal info or messing with your site.
Oh God,give me one more chance,i reglet all i did.And apologize to You the Most High.I have never been right to you and accept my apology Lord.Alikuwa ni Pastor John akiomba Mungu amsaidie katika wakati mgumu ambao alijitakia mwenyewe katika maisha yake.Aliishi kama mnyama japo alitumia jina la Mungu katika kujilimbikizia na kujiwekea utajiri mwingi kwa njia za giza.
Hakuwa na roho ya huruma wala wema,wachache walimuona kama Mungu,wengine walisema ni mtume wa Mungu alietumwa na Mungu kuja kuokoa wanadamu.Wengine walisema ni Shetani amekuja duniani baada ya kukosa malisho yake huko Ahera.Hakuna aliyejua ukweli wake au nini lilikuwa lengo lake.
Alifanya mengi makubwa siku za mwanzoni na kila mwenye kumsikia alitaka kumuona na kumshudia kwa macho yake.Aliponya wagonjwa na kusaidia vilema na vipofu.Hakuwa na jumba kubwa alilotendea mambo haya bali alikuwa na kibanda kidogo ambacho watu walikusanyika na wengine walika chini ya miti wakila neno la Mungu.
John,kijana wa mwisho katika familia yao na ndie anayetegemewa sana wa wazee wake hasa baada ya kaka zake wanne kuwa wahuni na wapiga debe maarufu.Kaka yake mkubwa aliitwa Juda,huyu alikuwa mtumiaji mzuri sana wa madawa ya kulevya na alikosa msaada baada ya madawa hayo kumzidi na alifariki dunia.
Ni kama hana Bahati mzee KIbabu kwani watoto wengine wote ukitoa John ni mateja...yani wanatumia madawa ya kulevya sana na wameshakuwa waathirika wa kutupwa wa madawa hayo.KIjana John alihudhuria shule vizuri ila hakupata bahati ya kufaulu sekondari.
Alihangaika na maisha akiwa anasaidia familia yake isiyojiweza kwa shida na taabu nyingi.Alianza kusukuma mkokoteni.Alikuwa maskani moja inaitwa sukuma twende.Pale alikuwa hana mkokoteni wake na alitumika kama kibarua wa watu waliomiliki mikokoteni ile.Haikuwa kazi rahisi kwani mara kwa mara aliugua sana mgongo na viungo vingine vya mwili.
Ilibidi aache kazi hii baada ya kuugua T.B ugonjwa ambao alishauriwa na daktari kutofanya kazi ngumu na hii ilikuwa kama kummaliza kiuchumi yeye na familia yake.Walianza kuishi kwa shida sana huku wakitegemea biashara ndogo afanyayo mama ya kuuza maandazi na mikate ya kumimina huko kwenye magenge.
Kupata pesa ya dawa ilikuwa ni vigumu,pesa kidogo aliyopata mama yake iliwasaidia kwa mahitaji kidogo ya nyumbani na haiutosha kununua dawa za kumtibu John.Aliteseka sana na mara kadhaa alienda kwa watu kuomba misaada ya pesa na chakula.
Baada ya kupata nafuu,John alienda kwa mwenye duka mmoja kuomba kazi yoyote ili aweze kujikimu yeye na familia yake iliyokuwakwenye hali ngumu.Mwenye duka alikuwa ni Muarabu ambaye alikubali kumapa kazi japo ilikuwa ngumu lakini alikubali ili kuweza kusaidia familia yake.
Alianza kazi kama mbeba sementi na kuli wa vitu vizito,alishusha mizigo kutoka kwenye malori na kupeleka store.Alimudu kazi hii kwa shida na alipata pesa ya kujikimu kwa shughuli hii.
Akiwa kazini na wenzake,aligundua kwamba wenzake wanafanya pia wizi ambapo mteja akija dukani kununa bidhaa nyingi,humuongeza na nyingine na walipata pesa zaidi kwa wizi huo.Hakuelewa mwanzoni walipanga vipi ila alijua ni kazi yenye hatari na inaweza kumpeleka kifungoni muda wowote.
Ili kuficha siri ile,wenzake walimfundisha wizi ule ili asijetoa siri kwa bosi wao pindi atakapoona mambo yale yakiendelea.Walimuonya kuwa makini na mwangalifu.Pia walimtishia kifo endapo endapo angetoa siri ile.
Siku moja alikuja mteja pale dukani na kumuulizia Dulla,John alimwambia kwamba Dulla ni mgonjwa na hayupo kazini siku ile.Unaweza kunisaidia,nataka kununua mifuko 200 ya sementi na ukiweza nitanunua mifuko mia moja kisha mifuko mia moja nitakupa nusu ya bei yake.
Alifikiri kwa muda John kisha akasema ngoja wajaribu na kuona kama ingewezekana.Mtejayule alienda hadi dukani kisha akalipia mifuko 100 ya sementi.Wakati wa kupakia,John alipakia mifuko mia mbili na mteja yule akaondoka na kumuahidi pesa yake jioni.
Alikutana na mteja yule na kupewa ujira wake.Alishangaa kuona kumbe anaweza kupata pesa nyingikwa siku moja endapo angeweza kupata wateja kama wale wengi zaidi kwa siku.
Baada ya muda upatao mwaka,mwenye duka aligundua hasara ya mamilioni ya pesa.Alitafakari sana juu ya hasara ile na akaamua kufanya uchunguzi wa kina bila ya kumjulisha mtu yoyote.Alipanga kuanza kuwacunguza wafanyakazi wake na kisha mtoto wake ambaye muda mwingi hushika pesa za dukani na kufanya mahesabu ya siku.
Alipanga mbinu mbali mbali ikiwemo kuweka kamera kwa siri pale dukani ili aone kama ni mtoto wake ndie huiba pesa pale dukani.Siku hiyo alisema hata kaa dukani na wanae kawa ndio muuzaji.Pia alitumia baadi ya rafiki zake kwa kuwapa pesa ili waje kujaribu kuongea na makuli wake kama wanaweza kutoa mzigo zaidi ya idadi ya mteja anayolipia pale dukani.
Alifanikiwa kumfuma John akiuza mara tatu ya mzigo uliolipiwa,yani alikuja mteja akitaka bati themanini,kisha akasema atalipia bati ishirini na bati sitini angemlipa John kama wangeridhiana.John hakuona tatizo na aliridhia bei na akatoa mzigo.
Baada ya kama dakika tatu tu toka apokee pesa toka kwa mteja yule,walikuja polisi na kumkamata na kumpeleka kituoni ambapo John alifunguliwa mashataka na kuhukumia miaka mitano jela na kazi ngumu.
Huko Jela John aliishi kwa shida sana,alikuta watu waliokaa miaka mingi jela na walimtesa sana na kumnyima godoro la kulalia.Siku moja usiku,alikuja mfungwa mmoja na kumuomba John akalale kwake kwani kulikuwa na baridi sana na John kama kawaida alikuw amekaa chini sakafuni na hakuwa hata na shuka la kujifunika.
Alikubali wito ule na kudhani huyu alikuwa ni msamaria mwema na mtu mwenye huruma.Mida ya saa saba usiku alishtuka na kukuta mfungwa yule akiwa uchi kama alivyozaliwa huku akimwambia John amlipe ujira wa kulalia kitanda chake.Kwa kawaida hapa kulala usiku mmoja ni bao mbili...na kama hutaki basi naita wafungwa wengine tunakukamata halafu tunakufanya kwa nguvu....alisema mfungwa yule.
John alijua ni utani,lakini alishangaa kuona mfungwa yule akiwa na munkari mkubwa huku uume wake ukiwa umesimama kama mtu aliyekosa tendo la ndoa kwa miaka tisa.Kjana sema moja..unalala hapa au niite wale watu wangu waje.Na wakija ujue kila mmoja atakula vitu leo na itakuwa ndio zamu kila siku leo kwa huyu kesho kwa yule.Ukinikubalia mimi nitakulinda na utakuwa mke wangu tu.
John aliwahikusikia maneno kama haya yakiwa yanasemwa mitaani tu,sasa anashuhudia mwenyewe na alikata shauri kuwa ni bora waje wengi na watumie nguvu kuliko kkukubali.Aliamini pia akipiga kelele basi askari magereza wangesiia na kuja kumsaidia.
Kama utani mfungwa yule alisema neno moja tu.."chakulaaaa" na ghafla walikuja wanaume kama saba hivi wakiwa uchi wa mnyama.mmoja wao akauliza wapi chakulaaaaaa,Yule mfungwa alitoa hifadhi akasema hii hapa chakula ila nanza mimi.
Baada ya maisha ya dhiki na magonjwa mengi,Baba yake Johnalifariki dunia,John hakupat taarifa za msiba ule na hata angepata taarifa basi asingeweza kuhudhuria mazishi yale.Mama yake John aliishi kama mjane kwa muda wote na shida zilizidi sana akaamua kuhamia kijiji kingine ambapo kulikuwa na eneo la kulima mazao kama mahindi,mtama na maharagwe.
Haikuwa rahisi kwa mama yake John kulima kwani alikuwa mtu mzima sana na nguvu zilishatoweka kabisa.Alimkumbuka sana mwanae na kulia kilasiku huku akimuombea maisha marefu na kifungo kisicho na mateso makali.
Akiwa ameshikwa na wanaume wapatao kama saba hivi,Johnalipiga sana kelele kuomba msaada lakini hakuna aliyesogea kumsaidia.Walimvua kaptura yake na ghafla walishangaa kuona John anawazidi nguvu na kukaa pembeni.Walistaajabu sana kwnai kila aliyemsogolea,alijikuta akirushwa kama bua kavu la mahindi na kuanguaka pembeni.
Ikawa story ambayo ilizagaa gereza zima kwamba kuna kijana ana nguvu kuzidi simba.Hivyo ndivyo alivyopona John kutoka kwa mikono ya mababa tisa yaliyoshiba ugali wa magereza na walio na uchu wa kufanya uasherati hata na wanaume wenzao.
Mwishoni Johnalimaliza adhabu yake na kutoka gerezani akiwa na magonjwamengi sana yakiwemoya ngozi,maralia na maognjwa yatibikayo.Alipata msamaria aliyempeleka hospitali na kutibiwa vizuri kisha akaanza kazi ya kuwatafuta wazazi wake.
Hakuna aliyethubutu kumwambia juu ya msiba wa baba yake.Kila mtu alimsaidia kumwelekeza mama yakealipo na ndipo alipofika kijiji kingine na kumkuta mama yake akiwa mgonjwa sana.Baba yako alifariki John na mimi naona umekuja kuniaga.Baada ya maneno yale mama yake naye alifariki.
Baada ya kurudi mjini,akiwa hana hili wala lile,alitembea siku moja hadi viwanja vya soko kuu la kariakoo.Kisha akawa anatembea kwenda maeneo ya magomeni kwa miguu kwakuwa hakuwa na nauli ba basi.Kufika maeneo ya Jangwani alikuta mkutanowa injili,hakusita kusogea na alikaa pale muda tu akiwa anatega sikio kwa makini.
Baadae mhubiri yule kutoka Nigeria alianza kutoa maombi maalum kwa wenye shida mbalimbali na akaombea wagonjwa na wenye ulemavu.John alipata hamasa na kujikuta akienda pale mbele ya umati wa watu na kutaka aombewe.
Siku ya mwisho ya mkutano ule ambao John alihudhuria siku zote,alimuomba mchungaji kama na yeye anaweza kuokoka ili awe mwana wa Mungu aliye msafi rohoni.Mchungaji yule alimpokea John na kumuombea,kisha akamkabidhi kwa mchungaji wa kanisa la pentekoste hapa Tanzania na kumuomba amsaidie kwa kadiri ya uwezo wake kwani aliamua mwenyewe kujitoa kwa Mungu.
Alianza masomo ya Injili na kupata shahda ya uchungaji ambapo hakukarimiwa karama ya uponyaji.Hii haikumpa umaarufu sana kwanialikuwa na waumini wachache na hakuweza hata kujimudu kutokana na sadaka za waumini hao.
Mungu hutenda maajabu pale watu wasipo stahili,unapokata tamaa ya kufanya jambo ambalo ni la manufaa ndipo hutokea msaada wa dhati kuleta neema na fanaka mbele yamacho yasiyo na matazamio.
John alipata mwaliko wa kwenda kuhubiri katika nchi kadhaa za Afrika.Alialikwa kwenye semina Uganda na Kenya.Alizuru nchi mbalimbali Afrika na aliona jinsi wachungaji walivyo na uwezo wa kuombea watu na kuwaponya magonjwa mbalimbali.Kwanini sio mimi John..alijiuliza siku moja huku akiongeza maombi kwa Mungu ili apate karama hizo.
Akiwa mwenye kukata tamaa,John alipata mwaliko wa kwenda Nigeria kutoa na kujifunza neno zaidi.Alikuwa ni yule mchungaji aliyemuokoa na aligharamia kila kitu ili John akatembee na kujifunza mambo ya uponyaji huko Nigeria.
Aliwasili Nigeria na kupokewa na mwenyeji wake kisha sikuiliyofuata alikaribishwa na waumini.John kijana mpole sana,huwezi kujua anawaza nini akiwa anatafakari.Alikuwa na karama ya maneno ya busara na kwa kipindi kifupi aliijua Bibilia sana.
Alipelekwa kwa wazee wa kinigeria ili wamuombee kwa Mungu awe na karama ya uponyaji na miujiza.Aliona ni bahati ya pekee na alimshukuru sana Mchngaji Jacob ambaye ndie alimpokea na kufadhili safari yake ya Nigeria.
Wazee walianza kumuombea na kama ungekuwepo basi hata weweungeungana na mimi kusema haya hayakuwa maombezi bali ni kukabidhiwa mifuko ya uchawi.
Alipelekwa juu ya mti mkubwa sana,kisha akaambiwa huko Mungu huwa karibu na binadamu na ukiomba tu unapewa kadiri ya maombezi yako.Akapewa fimbo ndogo sana na kuambiwa awe nayo kila mahali.unaweza kuiweka mfukoni na mtu asiione hata akikupapasa.
Kisha akakabidhiwa kibuyu kikubwa ambacho alitakiwa kukifukia kwenye eneo la kanisa lake.Na akiwa anataka kwenda kahali nje ya eneo la kanisa lake ni shrti amwage maziwa na nyama mbichi juu ya eneo lile alilofukia kibuyi kile.
Kisha akalishwa nyama ambayo hakuambiwa ni ya nini,akala kisha akapewa na sanamu ndogo sana aliyotakiwa akiwa analala lazima aifukizie ubani mwingi hata kama ni mchana au ugenini.
Alikabidhiwa mengi sana ya ajabu na kuambiwa sasa yupo fit kuanza miujiza....Ukiona mgomjwa wewe mtaje Mungukisha sema maneno yasioeleweka na utaona watu wakianguka na mapepo yakitoka.Unauwezo wakuona wachawi na watu wabaya.Wewe ni zaidi ya wachawi wote,wewe ni nusu ya Mungu,wewe ni shujaa wa vita ya anga hili.Alisema kikongwe mmoja huku akimshika kichwa John.
Baada ya siku kadhaa juu ya mti,Johnalishushwa na kupewa masharti magumu sana.Alitakiwa kutoa sadaka ya mtoto mchanga kila wano wa mwaka...tena awe mtoto ambaye si wa damu yake bali wa muumini wake anayempenda sana.
Alitakiwa kuhakikisha anafnya mapenzi na wanawake zaidi ya hamsini kutoka katika kanisa lake.idadi hii ni ya kila baada ya mizei sita yani wanawake waumini wake mia moja kwa mwaka.Hakutakiwa kufanya mapenzi mara tatu na wanawake hawa.
Alitakiwa pia kutokula kitu chochote kinachotoa damu.kama nyama,samaki nk.Alitakiwa kutooa kabisa kwani akioa tu ingekuwa ndio mauti yake.Alipewa masharti mengi tenakwa maandishi na akawa kazi yake ni kuyafuata tu.
Kule kanisani kwake John hakuaga anaenda wapi,watu walisema amekimbia shida,wengine wakasema ametoweka kimiujiza,na mengi yalisemwa juu yake.
Baada ya miezi miwili,Johnalirudi huku akitangaza kuwa alichukuliwa na Mungu kwenda kupewa ufunuo.Alianza kufanya miujiza na mambo mengi yaliyowafanya watu waamini kweli alitoka kwa Mungu na wengine wakahoji ni nguvu za giza.
Katika tukio moja,John alikuwa akihutubia mikoani na hapa alikuwa mkoa wa Arusha.Huko aliwaaibisha watu wengi hasa wapita njia kwa kusema yule yupo uchi..njoo hapa kabla sijakuaibisha mama..alisema hayo pale Arusha maeneo ya sekenke.Mama mmoja alikuwa anapita karibu na uwanja wa mpira alipokuwa anahubiri Mchungaji John.
Mbona unatembea hivyo mama,alimuuliza John yule mama mbele ya umati wa watu wapatao elfu kumi na moja na miatisa hamsini na tatu.Mama alijiinamiakwa aibu huku akilia tu.Omba Mungu nawe uokoke Mama haya vaa kanga hii na uendezako.
Pia alisaidia vilema na wengi walitembea,alianza kutimiza masharti ya kuzini na wanawake waumini wake na alimudu kwani alitumia njia za kudanganya anatoa mapepo na aliwabaka wengine na kuwafanya matendo ya ajabu sana.
Katika tukio moja,Johnalimtongoza mke wa katekista wa kanisa lake,mama huyu alikuwa mchamungu haswa na alimwamini sana mchungaji John.Hakuweza kujua ni kwanini alikuwa anamtaka kimapenzi.Unajua nimeolewa lakini Mchungaji,na Mume wangu ni rafiki yako na katekista wako pia ...akisikia itakuwaje jamani?alihoji mke wa katekista huku akihisi mchungaji anampima imani tu.
Lakini baada yamuda wa siku kadhaa alihisi labda mchungaji yup serious na akaamua kutomuangusha mchungaji hivyo alimpa tunda wakafanya uasherati kwa siri yao wenyewe na Mungu wao akiwaona tu.
Mchungaji Johnaliendelea kutoa neno la Mungu huku akikusanya vito na vitu vya thamani kama cheni za dhahabu na pete akidai madini ni vitu vya shetani alidai kuwa anakwenda kuviombea na kuchoma moto mbele yao.Kumbe aliuza vile vito vya thamani na kweli kicha akaleta vitofeki na kuteketeza kwa moto mbele ya waumini.
Siku moja John alimbaka muumini wake mmoja ambaye alikuwa ni mke wa mwanajeshi.Mwanamke yule aliondoka na kuhama kaisa bila kumwambia mumewe sababu ya kuhama kanisa.Alihamia kanisa la jirani na alimwambia mchungaji wa kanisa lile yaliyompata.
Ilikuwa ni vigumu kwa mchungaji wa kanisa alilohamia Mama yule kuamini maneno yake.Hasa ukizingatia alikuwa anamuheshimu sana Pastor John na kuamini alifanya yote yale kwa uwezo wa Mungu.Alitafakari na kuliweka kapuni suala lile.
Mchungaji John hakuwa na huruma hata kidogo,alijilimbikizia mali nyingi sana alizoziweka kwa rafiki zake ama kutumia majina ya marafiki zake kama kivuli mbele ya macho ya watu.
Hakuachakuwaponya watu na hii ilimletea waumini maelfu kwa maelfu.Siku moja akiwa Kwenye mahubiri yake,ghafla alitokea mzee mmoja wa makamo hivi na alikuwa anapita njia tu.Mzee simama na piga hatua tatu nyuma kisha moja mbele halafu kaa chini.Alisema Pastor John akimuamuru mzee yule kufanya atakayo.
Marehemu mama yangu aliwahi kunipa hadithi nyingi sana za mambo ya kutishatisha na aliwahi kunipa hadithi moja ya kuhusu wachawi ...kwamba huwa wanajuana na huzidiana nguvu wakati mwingine.
Mzee yule alipayuka kwa nguvu na kusema"enyi makutano...mnakutana kushuhudia uchawi ama mnataka utakaso?NI kijana mdogo sana huyu lakini ni mbaya sana.Anawadanganya tu na mnaweza kwenda motoni wote kama mkiendelea kumsikiliza huyu mchawi.
Maneno yale yaliwashtua makutano na wengine walidhani mzee yule anaropoka tu na wengine walioonja joto ya jiwe waliamini na wengine walibaki njia panda wasijue ukweli nini na uongo ni nini.
Nakuamuru uokoke mara moja.Ana mapepo huyu jamani na ngoja niwaonyeshe alivyo na uovu mwingi..alisema Mchungaji John huku akimsogelea yule mzee.Ghafla mzee alianza kupiga kelele na kutaja majina ya watuw wengi na waliofahamika.Wengi walikuwa ni marehemu na kila mtu alipata mshangao na kuanza kumuamini Pastor John.
Aliendelea na mambo yake huku akiendelea kufuata masharti aliyopewa kule Nigeria na aliendelea na kazi ya uponyaji pia.Ukiachilia maovu kama kubaka na kuzini na wake wa waumini wake,alisaidia watu walokuwa na shida mbali mbali na pia alikuwa mtu aliye Mkaribisha Mungu mbele za watu pamija na kwamba alifanya mambo hayo kwa njia za giza.
Sultan Kauche,kijana wa miaka thelathini na tano,baada ya kuwa jamabazi na muovu wa kutupwa,alisikia habari za Pastor John na aliamua kwenda kumuona wa Ushauri na kuokoka pia.Mkewe anaitwa Aisha na woteni waisilamu wazuri tu.
Aisha alikuwa na mapepo mabaya na hakuwahi kujua kama alikuwa na apepo yale.Hayakupenda kabisa kuona misalaba wala kuona mtu mwenye Bibilia,Wakiwa kwa Pastor John,aligundua kuwa Aisha ana mapepo makali ambayo aliyakumba akiwa mtoto mdogo na ni mengi ajabu.
Hakutaka kumtisha bali alimwambia Sultan wapate faragha wanaume kidogo na ndipo alipomwambia kwamba mkeo ana mapepo makali sana na mengi sana.Sikutaka ajue habari hii kwani ingemnyima raha sana.Tukianza kuwaokoa tu yatapanda na itabidi wawepo watu wengi wa kumshika.
Yananguvu sana mapepo ya aina hii,pia hayaja wahi kuchokozwa sasa ni mashujaa haya na itabidi tuyatoe tu.Walipanga siku ya kufanya wokovu na kutoa mapepo yale.Ilipowadia siku hiyo,walifika kaisani na kukuta watu wameandaliwa tayari kwa kazi ile ngumu na walianza kuimba kama kawaida yao.
John alitoka akawaacha wanaimba kisha aliingia chumbani na kuomba mauchawi yake yafanye kazi kama anavyotaka,kisha akayapa maziwa na nyama mbichi majini yake na kuja tena mbele za watu akiwa na sura iliyobadilika sana.Kama mtu mwenye hasira na alikuwa na nguvu ajabu.
Akamshika kichwa Aisha nakusema..."Mungu aliwaleta duniani kutesa wanyonge na wasio mwamini,Aliwapa uwezo mkiwa chini ya mamlaka yake kisha akaanza kuongea vitu visivyoeleweka"Ghafla Aisha alianguka chini na kuanza kujipiga piga ukutani na sakafuni kama anataka kuakata roho.
Alipiga kelele sana na watu walijaa kushuhudia maajabu haya.Alihangaika kama muda wa masaa saba hivi na mapepo yale yakaaga na kuondoka.Ndipo Mchungaji John akijidai anamtukuza Mungu kwa kazi yake ya ajabu na akaenda tena chumbani kwake ambapo hakuna mtu aliyewahi kuingia huko.
Baada ya siku kadhaa,Aisha na Sultan walikuwa waumini wazuri sana wa John,uda mwingi Aisha alikuwa akiutumia pale kanisani kufanya vikazi vidogo vidogo na kumsaidia Pastor John shughuli mbali mbali.
Kama kawaida yake Pastor John hakusita kumuomba kufanya tendo la ndoa Aisha ambaye alikubali ili kulipa fadhila za kutolewa mapepo yale.
Siku ya kufa nyani..miti yote huteleza kwani haikuchukua muda sana kwa watu kuanza kuhisi mahusuanao ya mchungaji huyu na wanawake kadhaa...Watu walijiuliza inakuaje mtu wa Mungu kuanza kuzini..tena na wake za watu jamani??
Mchungaji John alinogewa na Penzi la Aisha akachonga mbuyu na kuvunja masharti aliyopewa kule Nigeria.Alizini na Aisha zaidi ya tanomara hamsini na taratibu uwezo wake wa kufanya miujiza ulipungua.
Alishangaaa kunoaa anadhulumiwa mali zake na marafiki walioaminiana sana na waumini walianza kukosa imani naye.Wengine walidhani anapumzika kufanya miujiza na kuponya watu.Wengine walisema nguvu zake za giza zimeisha nguvu na mengi waliyoyasema kwa muda wao.
Aliamua kutangaza kupumzika na maombezi kwakuwa alikuwa amechoka sana.Alipanga kurudi Nigeria ila cha ajabu ni kwamba pesa zake zilitoweka kwa njia ya ajabu sana.Kila alipoenda bank kuchukua pesa,basi akishika mkononi hugeuka karatasi na akiweka kwenye pochi huwa zinatoweka tu.
Aliendelea kuona mambo ya ajabu yakimtokea huku umaarufu wake ukizidi kwa kujulikana ilikuwa janja ya nyani tu na wengi walianza kumkimbia na kusema alikuwa anatumia nguvu za giza.
Alipoteza imani haraka sana mbele za watu na hakufanikiwa hata kupata nauli ya kwenda Nigeria.Wale aliowadhihaki kwa kuwaita wachawi na washirikina walitumia nafasi hii kulipiza kisasi kwani walianza kumlimisha sana usiku akiwa amelala na ilifika kipindi akawa anaamka na kujikuta yupo mjini tena uchi.
Siku moja alijikuta akiwa njiapanda ya kwenda kanisani kwake asubuhi siku ya jumapili na akiwana nguo ya ndani tu.Alikuwa kama aliyechanganyikiwa huku akiwaomba msamaha waumini wake na kutana maovu yake bila yeye kujua anayosema.
Baada ya kupata fahamu,aliamka na kukimbia bila kujua anaelekea wapi.Aliamua kuhama mji na hakuna anayejua alip hadi leo ila kuna funufunu kuwa yupo sumbawanga akijaribu bahati yake kwa mara ya pili.
Pastor John,mimi PJ nakushauri uache kufanya hayo ufanyayo na umrudie Mungu kwani Kizazi hiki hakijaona muujiza wowote na hakitaona muujiza hadi hapo Mungu mwenyewe akipenda.Nakushauri ujirekebishe na umrudie Mungu na umpendeze katika siku zako zilizobaki.
KAMA IKIMPENDEZA BWANA...NASEMA
ALAMSIQ
I DEDICATE THIS STORY TO THE LATE MY MUM STELLA CHALLE...REST IN PEACE MUM.I MISS YOU AND YOUR LOVE MUM.I WILL ALWAYS REMEMBER YOU,PRAY FOR YOU AND YOU WILL ALWAYS BE THE WOMAN I LOVE MOST.YOUR FAMILY MISSES YOU MOM,YOUR DAUGHTERS...EMMY,NGÌNA,JOSE AND YOUR HUSBAND RICHARD.
REST IN PEACE BELOVED MUM.DIED 19.11.2005