Stay Signed In
Do you want to access your site more quickly on this computer? Check this box, and your username and password will be remembered for two weeks. Click logout to turn this off.
Stay Safe
Do not check this box if you are using a public computer. You don't want anyone seeing your personal info or messing with your site.
Alibadilika ghafla Sauda na aliamua kukata mawasiliano na mimi.Nilipompigia simu hakupatikana na nilihisi labda ni kwaajili ya harusi aliyohudhuria huko Arusha.
Baada ya siku kama nne toka harusi ipite,nilipiga tena simu na kuongea na Sauda,alijibu kama mtu asiyetaka kuongea na mimi.Huku akiwa na maringo kibao na majivuno alisema namtafutia nini?Nimepiga simu kukujulia hali tu Sauda na si kwa nia nyingine kama simu yangu si ya muhimu kwako basi kata,nilimwambia na kweli aka kata simu na kuizima kabisa.
Sikuona sababu ya kulazimisha mapenzi japo niliumia sana moyoni,niliamua kukubali matokeo yale baada ya dharau na majivuno aliyonionyesha Sauda.Maumivu niliyokuwa nayo moyoni hayakuwa na kipimo kwani ni muda wa siku tisa tu zimepita toka nimemtambulisha Sauda kwa wazazi wangu.
Mama na Baba yangu walimpenda sana Sauda kwani alikuwa mpole na mwenye tabia nzuri tu kwa mwonekano wake wa nje.Nilihisi labda ananipima tu kwani alikuwa anafanya yote haya huku anatabasamu kubwa sana usoni.
Niliona nisiwashtue wazazi wangu sababu sikuwa na uhakika kama Sauda atarudi kundini ama ndio amenitoka kimoja maana kuna wakati nilihisi angerudi kwani alinipigia simu na kusema hujambo GOD?
Mishi ni rafiki mkubwa sana wa Sauda na nilikwenda kwake nikiwa napelelza habari za Sauda nijue nini kilimsibu maana mara nyingi Sauda alimtumia Mishi kuja kwangu tulipokuwa na mikwaruzo kadhaa.Niliamua kufanya hivyo ili kuuridhisha moyo wangu uliokuwa unasononeka kwa uchungu na mawazo mengi juu ya Sauda.
Naitwa Godfrey Mwalukingwe,ni mzaliwa wa mkoa wa mbeya na ninaishi hapa hapa mbeya.Ni mwajiriwa wa kampuni ya TrC ambayo hutoa huduma za usafirishaji abiria na mizigo kwa njia ya gari moshi..wenzetu huita train.
Katika maisha yangu nimewahi kuwa na mahusiano machache sana ya mapenzi na hii ni kutokana na hali halisi ya maisha na gonjwa hili linalotishia na kuhatarisha maisha ya watu hapa duniani yani UKIMWI.
Nilikutana na Sauda nikiwa kwenye sherehe ya mfanya kazi mwenzetu pale Mbeya ambaye anaitwa Abel.Alikuwa anaoa na nilihudhuria nikiwa na rafiki yangu kipendi David.
Tukiwaharusini,tulikutana na watu wengi sana,warembo kwa mabibi,vijana kwa wazee,watoto na wote unaoweza kutoa wasifu wao kama binadamu aliyepo kwenye sherehe ya rika zote.
Katika kufahamiana na huyu na yule,ndipo nilipojikuta namkanyaga dada mmoja aliyependeza haswaaaaa.Haikuwa nia yangu wala sikutarajia kufanya hivyo ila ilitokea nikamkanyaga mggu wake wa kushoto na kumuumiza sana.
Nilimuomba radhi kisha nikamchukua hadi nilipo paki gari yangu na kutoa dawa kadhaa na kumpaka mguuni.Alivimba mguu,unajua tena dada zetu hawa ngozi lainiiii basi nilimchua huku nikimfariji kwa maneno ya furaha na alipokea msamaha wangu na akataka kurudi ukumbini shereheni.
Nilimuuliza kama alikuja na mtu pale ukumbini akasema alikuja pake yake hapo nikajua marembo huyu ni single kwa vyovyote vile.Tulifika ukumbini akawa amekaa karibu na mimi na nikampa ofa ya kumpeleka kwao kama angependa naye bila hiyana akasema akichoka tu ataniambia.
Tulijikuta tukiwa tunahadithiana mambo ya maisha huku tukia hatuna habari ya nini kinaendelea shereheni.Tulipeana story kibao hadi ikafika wakati mimi nikasahau kama nimetokea kumpenda huyu Sauda.
Wasifu wake wa nje ulikuwa asilimia 99%kwani hata mwalimu afundishapo darasani hawezi mumpamwanafunzi uwezo wa aslimia mia moja bali hubakiza sehemu ambayo mwanafunzi hujazia kutoka vyanzo tofauti.Nmi nikatoa asilimia hizo kama mwalimu ili asilimia moja hiyo uitafute na wewe kama ukiikosa abaki na hiyo 99%.
Muda ulifika ambapo Sauda alitaka kwenda nyumbani kwao,Abel alikuwa hoi kwa mapombe aliyokunywa pale harusini na alitamani muda wowote twende nyumbani.Tuliondoka na kushika njia ya mjini kama tunaenda mwanjelwa vile.Kufika sokoni tukakata kushoto na kuingia maeneo ya Veta.
Nashukuru kwa kunifikisha nyumbani na usijali nitapona tu mguu.alisema Sauda huku akiwa anashuka garini.Natumaini tutazidi kuonana na nitakutembelea siku yoyote kuona maendeleo yako dada.Mie nilisema kwa adabu kubwa.sikutaka papara kwani siku ya kwanza mtu hutakiwi kuwa na papara ya kutaka kumaliza shida zako zote.